SIMANZI na vilio vilitanda katika familia ya mwalimu John
Frayo baada ya watoto wao wawili Lucas John(4) na Emmanuel John (2.5) kutumbukia ndani ya kisima cha maji na
kupoteza maisha.
Akizungumza tukio hilo, Diwani wa kata ya Kisarawe 2, Issa
Zahor alisema lilitokea jana saa sita mchana mtaa wa Vumilia Ukooni, wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam ambapo
watoto hao walitumbukia katika kisima chenye urefu wa futi tatu kilichopo nyuma
ya nyumba waliokuwa wakiishi.
“Watoto walikuwa wakicheza na bahati mbaya walitumbukia
katika kisima kilichopo mita 50 nyuma ya nyumba waliokuwa wakiishi na familia,”
alisema Zahor.
Alisema kuwa baada ya kuwatoa walikimbizwa hospitali ya
Vijibweni, daktari wa zamu alithibitisha
kuwa tayari walikuwa wamekwisha kufariki.
Zahor alisema kuwa kutokana na matukio kama haya kujirudia
ameamua kuitisha kikao cha viongozi wa serikali za mitaa ili kujadili namna ya
kuepuka vifo hivyo.
“Tukio hili ni la pili ndani ya mwezi mmoja tumepoteza
watoto wanne ambao wangekuwa ni nguvu kazi ya Taifa baadae, nimepanga kuitisha
kikao cha ODC tuongelee jinsi tutaa,”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni