Jumatano, 13 Mei 2015

MAFURIKO YAUWA ASKARI JWTZ



ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ) Lugalo,  Barnabas Mataja(48) amefariki dunia baada kusombwa na maji katika  mto Mzinga.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ACP Japhari Mohamedi alisema tukio hilo lilitokea Mei 11 katika eneo la Kimbangulile,Kata ya Tambani, Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Mohamedi alisema juzi marehemu alikuwa akirudi nyumbani kwake akitokea matembezini  wakati akivuka mto huo maji yalimzidi nguvu na kusombwa.
“Mwili wa marehemu umepatikana jana saa nne asubuhi katika eneo la Tambani,” alisema Mohamedi.
Alisema mwili wa marehemu umechukuliwa na ndugu zake kwa ajili ya maandalizi ya maziko.

  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni