DIWANI wa
kata ya Kisarawe II, Manispaa ya Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam, Issa Zahor
amewataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi kuvunja makundi ndani ya chama hicho pindi tu
kura ya maoni inapomalizika.
Akizungumza
na MWANDISHI wa blog hii jana jijini hapa, Zahor alisema makundi ya kura za
maoni yanatakiwa kuvunjwa kabla ya kuingia katika uchaguzi mkuu.
Alisema
wanachama wa chama hicho wanapaswa kumuunga mkono mgombea aliyepita na si
kuhamia upinzani.
“Mara nyingi
makundi yamekuwa hayavunjwi kiasi ambacho yanakigharimu chama katika chaguzi
mbalimbali kwa upande mmoja kuunga mkono upinzani,” alisema Zahor.
Alisema
amelazimika kusema hayo kutokana na matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa
kuwashitua ambapo katika mitaa 11 ya kata hiyo, saba walichukua wapinzani na mitano
kuchukuliwa na CCM.
“Matokeo ya
upinzani kuchukua viti vingi vya mtaa kumetokana na kutokuwa na umoja ndani ya
CCM,” alisema.
Akizungumzia
kuhusu Ilani ya CCM, Zahor alisema ametekeleza kwa asilimia kubwa kwani amesimamia
uchimbaji wa visima kwa kila mtaa.
“Tumetekeleza
ilani ya CCM kwani mpaka sasa kuna kisima cha maji kila mtaa na kuwapunguzia
muda mrefu waliokuwa wakitumia kinamama kutafuta maji ,” alisema.
Alisema kwa
upande wa miundombinu pia wamefanikiwa kutengeneza barabara zinazoingia na
kutoka katani hapo pamoja na zile za mitaani.
Aliwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono
katika uchaguzi ujao ili akamilishe na kuendeleza mambo ambayo bado
hayajakamilisha pamoja na kutekeleza Ilani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni