Jumamosi, 9 Mei 2015

UTARATIBU MPYA WA KWENDA HIJA


UTARATIBU wa kusafirisha mahujaji wanaokwemda nchini Saudi Arabia katika mji mtakatifu wa Makha kwa mwaka huu umebadilishwa na wizara ya hija ya nchi hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Rais wa taasisi ya kusafirisha mahujaji ya AL jazzira international Hajj  trust Alhaj Seifu llah alisema Serikali ya nchi hiyo imeamua kuboresha mapokezi ya wageni wanaokwenda hija tofauti na zamani.
Alisema kuwa mahujaji wote wanaokwenda kuhiji taarifa zao zinatakiwa zipatikane mapema kupitia mfumo maalum wa kielotronik kupitia Paspoti zao ili ijulikane idadi ya mahijaji wanaoingia nchini humo kwa mwaka huu.
Alisema lengo la kutaka taarifa hizo mapema na kujua idadi yao ni kutaka kuboresha maandalizi ya mapokezi kwa mahujaji hao ili waongeze huduma katika maeneo watakayofikia.
 Seifu aliwataka wale wote walikaohitaji kusafiri wajitokeze mapema kujiandikisha katika taasisi watakazo safari nazo ili kuepuka usumbufu ambao usio wa lazima.
“Wizara hiyo imetoa siku ya juni 27 mwaka huu kuwa siku maalumu ya kuufunga mfumo huo hivyo hujaji yeyote atakaechelewa siku hiyo atakuwa si miongoni mwa watakaosafari.
Alisema kuwa kwa mwaka huu taaasisi yake ina mpango wa kusafirisha mahujaji kwa njia ya Gari kupitia Sudani  endapo hali ya usalama  nchini humo itakuwa ya kuridhisha.
Kwamwaka huu Al jazira itasafirisha mahujaji kwa dola za kimarekani 4400 na kuhiji kwa niaba ya mtu asiyejiweza ni dola 1500 hiyo inajumuisha pamoja na gharama zote kwa siku watakazo kuwa huko.
Hata hivyo aliwataka mahujaji wanaosafiri na taasisi hiyo kulipia katika benki za NMB kwa akaunti namba 20410001982 kwa watakaolipia kwa kutumia fedha za kitanzania na kwa watakaotumia dola za kimarekani akaunti namba 20410002001.
Ibad. a ya hija kwa waislamu ni moja kati ya nguzo tano ya dini hiyo




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni