Alhamisi, 14 Mei 2015

BAREGU AONYA HALI YA KISIASA BURUNDI



 BAREGU
 Mhadhiri wa Chuo cha Mtakatifu Augustino(SAUT), Profesa Mwesigwa Baregu amesema hali iliyojitokeza jana ya jaribio la mapinduzi nchini Burundi ilionekana ingeweza kutokea tangu awali kutokana na msimamo wa Rais Nkurunziza kuanza kuleta machafuko na uvunjifu wa amani.
Alisema viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) wanatakiwa kuendelea na jitihada zao za kumtaka Rais Nkurunziza kuachana na msimamo wake na kuhakikisha kuwa utawala wa Jeshi haujiandai kuota mizizi.
“Hali hii ilionekana inaweza kutokea…wanachopaswa kufanya viongozi wa EAC ambao nafikiri wataendelea na mkutano na rais Nkurunziza, ni kuhakikisha kuwa wanaleta suluhu mapema kwa kuweka serikali ya umoja wa kitaifa ili uongozi wa Kijeshi usijiandae kuota mizizi na uruhusu uchaguzi kufanyika kama ilivyopangwa, ” alisema Profesa Baregu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni