Kesi inayomkabili Mwimbaji wa nyimbo za Injili na mfanyabiashara Emmanuel Mbasha imeendelea leo katika mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa kumsikiliza shahidi namba sita,
Secherela Challo.
Shahidi huyo alitoa ushahidi wake jana mbele ya Hakimu
Flora Mjaya na Mwendesha Mashtaka Munde Kalombora.
Mbasha anadaiwa kumbaka shemeji yake (17) kati ya Mei 23 na
25, 2014 eneo la Tabata ambako alikuwa akiishi naye.
Septemba 5 mwaka jana binti huyo aliieleza Mahakama kuwa
alibakwa na shemeji yake huyo kwa awamu mbili tofauti kabla ya kufanikiwa
kukimbia.
Kwa sasa Kesi hiyo inasikilizwa Mahakamani hapo kwa siri kwa mujibu wa
Sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai ya mwaka 2003 sura ya 20 kifungu cha 186,
kifungu kidogo cha tatu ili kulinda haki ya binti huyo.
Tayari mashahidi watano akiwamo binti huyo, Flora ambaye ni
mke wa Mbasha.
Daktari aliyemfanyia vipimo wamekwisha kutoa ushahidi
mahakamani hapo ambapo alisema katika kufanya vipimo hakukuwa na ushahidi wowote ulioonyesha kuwa Mbasha alimwingilia kimwili binti huyo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 16, mwaka huu itakapotajwa
tena.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni