MVUA zawa
sababu za kusogezwa mbele kwa makabidhiano ya Mradi wa ujenzi wa daraja la kisasa la Kigamboni ambao
mpaka hivi sasa umekamilika kwa asilimia 80.
Meneja wa
mradi huo kutoka NSSF, Karim Mataka, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam kuwa wanatarajia ifikapo Desemba watakuwa wamekamilisha ujenzi lakini
mwishoni mwa mwezi Septemba au mwanzoni mwa Oktoba daraja linaweza kuanza
kutumika na watembea kwa miguu.
Alisema
changamoto mbalimbali zimechangia kwa asilimia kubwa kuchelewa kukamilika kwa
daraja hilo ambalo awali lilikuwa likamilike Januari 31 lakini kutokana na
baadhi ya changamoto zilizojitokeza ikasogezwa hadi mwezi Julai na sasa
wanatarajia kuukamilisha mwishoni mwa mwaka huu.
Alisema
mpaka sasa mradi huo umeshaghalimu bilioni 240 na kwamba baada ya kukamilika
ndio watataja gharama halisi iliyotumika katika ujenzi wa daraja hilo.
Aliongeza
kuwa serikali imeiruhusu NSSF kumalizia ujenzi wa barabara ya mapokeo kwa
kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 2 ile Vijibweni kwenda kwenye maungio
ya barabara ya Kibada.
“Pamoja na
changamoto zilizotufanya kuchelewa kidogo lakini tunashukuru tunaenda vizuri na
daraja letu litakuwa na barabara sita ambazo tatu zitakuwa zikitokea Kigamboni
na tatu zitakuwa zikielekea Kigamboni,” alisema Mataka.
Alisema
ujenzi wa daraja hilo linasimamiwa na wahandisi kutokana TANROADS, Wizara ya
Ujenzi pamoja na NSSF.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni