WAJENZI wa vibanda
vya biashara vinavyotengeneza uzio wa uwanja wa maonyesho wa sabasaba Morogoro,
wamelalamikia kunyanyaswa na Ally Issa, Katibu wa wilaya wa Chama cha
Mapinduzi(CCM) mkoani humo.
Akizungumza
kwa niaba ya wenzake mmoja wa wajenzi hao, Robert Mluge alisema mwaka 1989 walijenga
vibanda kuzunguka uwanja huo kwa
makubaliano na manispaa ya morogoro kuwa wao ndio watakuwa wamiliki wa vibanda
huku manispaa ikimiliki sehemu ya uwanja.
Alisema lengo lilikuwa ni kuweka uzio wa
uwanja wa maonyesho wa sabasaba ambapo
mjenzi alijenga kwa kuelekeza milango nje ili afanye biashara zake huku
manispaa ikiendelea na maonyesho ya sabasaba kwa ndani.
“Manispaa
ilitutafuta yenyewe kwa kutushawishi kupitia Afisa Utamaduni wa manispaa ya
Morogoro aliyejulikana kwa jina moja la Ntemo. Tulikubali kujenga kwa
makubaliano sisi kumiliki vibanda na wao kumiliki uwanja,” alisema Mluge.
Alisema
mnamo 2007 Chama cha Mapinduzi wilaya ya Morogoro waliwataka wajenzi hao kulipa
kodi ya pango ya shilingi 150,000 kwa kila kibanda kwa madai kuwa wao ndio
wamiliki halali wa uwanja huo.
Alisema
baada ya wao kukataa kuilipa CCM fedha hizo walivunjiwa vibanda vyao na
kunyang’anywa mali na vitu vyao kama mashine na majokofu na kuuzwa kwa mnada na dalali aliyejitambulisha kutumwa na CCM, G.
Mwambogela kutoka Majembe Auction Mart.
Alisema CCM iliwashitaki
wajenzi hao mara kadhaa katika mahakama na mabaraza ya ardhi na hukumu
zilionyesha kuwa wajenzi wanahaki hivyo kukitaka chama hicho cha siasa kuwarudishia
vibanda na kuwalipa mali zao walizoziuza.
Kwa mujibu
wa hukumu iliyotolewa na msajiri wa mahakama kuu kitengo cha ardhi L, M Mlacha,
imeeleza kuwa maombi yaliyotumwa
na CCM kwa ajili ya utekelezaji wa kuwafukuza na kufungua milango madai hayo hayana
msingi wa kisheria, ni potofu na awalipe gharama.
Baada ya
hukumu hiyo Wajenzi walimuandikia Katibu Mkuu wa CCM kumtaka amuamuru Katibu wa
wilaya wa chama hicho lakini mpaka sasa hawajajibiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni