Jumamosi, 9 Mei 2015

MAFURIKO DAR SI SALAMA.

WATU nane wameripotiwa kufariki dunia kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha  katika  jiji la Dar es salaam.
Taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Suleiman Kova, alisema watu tano wametambuliwa na wengine watatu bado hawajatambulika na miili yao imehifadhiwa katika ya Hospitali  ya Mwananyamala.
Alisema Mei  6 mwaka huu mnamo saa 1 usiku maeneo ya magomeni Wilaya ya Kinondoni  aliyetambulika kwa jina Shabani Idd(73) mkazi wa Manzese alisombwa na maji ya mto ng’ombe alipokuwa akijaribu kuvuka mto huo  na mwili wake ulipatikana Mei 7 akiwa amefariki.
“Kifo kingine kili tokea Mei 7  mwaka huu mnamo saa 6 mchana maeneo ya Mwanamnyamala  mbuyuni Masumbuko Douglass (50) alianguka na kufariki dunia ghafla wakati akitoa maji yaliyo ingia ndani kwake uchunguzi wa awali unaonyesha  alikuwa na tatizo la ugonjwa wa kifafa hivyo wakati akiangaika kutoa maji ugonjwa huo  ulimpata na kuanguka kwenye maji”alisema Kova
Alisema Rashidi Hassan(36) Mkazi wa Mvuruhana Pemba mnazi Kigamboni alizama katika mkondo wa maji unaoelekea baharini Mei 6 mwili wake ulipatika Mei 7 ukiwa unaelea  majini  umbali wa Mita 500 toka eneo alilozama.
“kifo kingine kimetoke Yombo Makangarawe Mei 6 mtoto Gloria Mrema mwenye umri wa mwaka moja na miezi mitatu alipotea baada ya watoto wenzake kumuacha wakati wakicheza kwa pamoja juhudi za kumtafuta zilifanyika bila mafanikio hadi mwili wake ulipopatikana ukiwa unaelea majini katika mto Mzinga akiwa tayari  amepoteza maisha mwili wake umehafadhiwa Hospitali ya Temeke”alisemaKova.
Alisema kifo kingine kilitokea Mei 8 mwaka huu Kinondoni Mkwajuni mtu mmoja mwanaume jina lake hali kufahamika anakadiwa kuwa na umri(40-45) alikutwa amefariki dunia mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi.
“Pamoja na vifo hivyo kuripotiwa pia  mtu mmoja Mabula Moses(65) mkazi wa vingunguti buguruni Wilaya ya Ilala amevunjika mguu wake wa kulia chini ya goti baada yakuangukiwa na ukuta wa ghala la Fida Hussen lilopakana na nyumba yake, majeruhi amepelekwa katika Hospitali ya Amana”alisema.
Alisema katika Kata ya Mchikichini taarifa ya mafuriko inaonyesha nyumba takribani 70 zimefunikwa na maji hadi juu ya paa ambapo wakazi wake tayari wamehama huku watu 35 wamejihifadhi Shule  ya Sekondari Mchikichini.
“ Kata yaJangwani zipo nyumba takribani zinakadiliwa kuwa 100 zimefunikwa namaji hadi juu ya paa watu 300 walihama mapema.
“Maeneo mengine  yaliyo athirika zaidi kutokana na mvua hizo ni Keko, Changombe maduka mawili ,Yombo vituka, Vingunguti , Africana,Msasani bonde la mpunga,Jangwani ,Manzese, Kigogo, Mburahati, Boko basi haya na maeneo mengine taarifa hazijapokelewa,”alisema Kova.
Alisema  wananchi wote kuchukua tahadhari ya hali ya juu hasa wale wanaoishi kwenye maenea ambayo ni mikondo ya maji au watumiaji wa barabara  zinazopitiwa na mikondo hiyo.
tuwasaidieni waathirika

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni