MTU mmoja
ambaye jina lake halikufahamika amepigwa risasi mbili na kuporwa fedha na mtu
mmoja anayedhaniwa kuwa ni jambazi katika eneo la Karibu na Deluxe Bar,
Sinza Kijiweni wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo
limetokea leo, katika maeneo hayo ambayo blog hii ilifika na kuelezwa kwamba tukio hilo lilitokea majira ya saa
sita mchana.
Dereva aliyekuwa akiendesha gari lililoshambuliwa lenye namba T 236
DDT alifahamika kwa jina moja la Abbasi alielezea
tukio hilo kwa kusema kuwa fedha ambazo majambazi hao
walichukua walikuwa wamezitoa benki moja iliyoko Mlimani City.
Dereva huyo
anasema kuwa baada ya kuchukua fedha ambazo hakuzitaja zilikuwa kiasi gani
lakini watu waliokuwa hapo walisema zilikuwa milioni 10, walitoka Mlimani City
na kuelekea katika hospitali ya mtaalamu wa watoto iliyopo Sinza.
“Baada ya
kuingia na kuegesha gari alitufuata mtu mmoja aliyekuwa amevalia koti jeusi
akiwa ameshuka kwenye pikipiki aina ya Boxer na alipofika alisogelea gari letu
na kufunua koti lake, lililokuwa na silaha aina ya SMG,” alisema.
Abbasi
alisema kuwa mtu huyo alimuelekezea silaha abiria aliyekuwa nyuma ya gari na
kumuamuru kutoa fedha, amri ambayo haikutekelezwa na mtu huyo aliyemueleza
kwamba hana fedha.
Abbas alisema baada ya
kuona anabishana nae alimpiga risasi ya kwanza, akageuza SMG kwangu nikakimbia,
akafyatua lakini hakunipata ndipo nikasikia risasi nyingine ikipigwa,” alisema.
Aliongeza
kuwa wakati anarudi alikuta majambazi hao walikuwa wameshaondoka na mkoba wa
fedha ‘Briefcase’ na kutokomea nao.
Hata hivyo tukio hilo la kushtukiza liliwafanya wasamalia wema pamoja na wananchi kumpeleka majeruri huyo hospitali .
Ingawa
kulikuwa na taarifa kwamba fedha zilizoporwa zilikuwa milioni 10, lakini Dereva
huyo alisema kuwa majambazi hao waliondoka na kiasi ambacho hata hivyo
hakikuwekwa wazi.
Askari
polisi walifika katika eneo hilo na kuzoa kipande cha utumbo kilichokuwa
kimedondoka sakafuni kikiwa na maganda matano ya risasi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni