MKAZI wa Kariakoo Mjini Dar es Salaam
Godfrey Kwikwilukiza (33),jana amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo
Kariakoo akikabiliwa na tuhuma za kujipatia kiasi cha fedha Sh 20,000 kwa njia
ya udanganyifu.
Akisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi
Christine Ruguru,Karani wa Mahakama hiyo Lucy Rutabanzibwa, alidai kuwa
mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Mei 23 mwaka huu eneo la Stesheni.
Rutabazibwa alidai Mahakamani hapo kwamba
mtuhumiwa alijipatia fedha hizo toka wa mtu mmoja anayejulikana kwa jina la
Shabaan Salum, kwa kudanganya kuwa yeye ni askari wa jiji.
Mshtakiwa
alikana kutenda kosa hilo na upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea ambapo
Hakimu alidai kuwa mshtakiwa anatakiwa alete wadhamini wawili wenye barua
kutoka serikiali za mitaa watakaoweka bondi ya maandishi ya Sh. Laki 1 kwa kila
mmoja.
Hata hivyo
mshtakiwa alirudishwa mahabusu kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo
kesi hiyo itakuja tena kusikilizwa hoja za awali Juni 11 mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni