HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imeingia makubaliano
na Jiji la Humburg la Uingereza kujenga
mtambo wa kuchakata taka katika eneo la Mabwepande.
Ujenzi wa mtambo huo utagharimu Sh
bilioni 3.5.
Hayo yalielezwa Dar es Salaam jana na Meya wa Manispaa
hiyo, Yusuph Mwenda wakati wa uzinduzi wa soko la wafanyabiashara wadogo Sinza.
“Tayari tumepata kiwanda ambacho tutakitumia kuchakata taka
za ‘organic’ ambazo zitatengenezwa mbolea ambayo tutaitumia kwa matumizi mbalimbali. Mradi huo tunatarajia utatengeneza ajira
zaidi ya 1,000,” alisema Mwenda.
Akizindua soko hilo, alisema litasaidia kupunguza idadi ya
wafanyabiashara wasiokuwa na maeneo maalum ikizingatiwa lina vizimba 512.
“Kunzia KESHO mnaruhusiwa kuanza kufanya biashara kwa sababu
soko hili tumelijenga si mapambo tunataka kukabiliana na changamoto ya
wafanyabiashara kutokuwa na maeneo maalum pamoja na ukosefu wa ajira. Vipo vizimba 512 kwa maana hiyo tutapunguza
kwa kiasi changamoto hii,” alisema.
Alisema manispaa hiyo pia imeanza ujenzi wa soko jingine
kubwa eneo la Mburahati litakalogharimu Sh bilioni 1.8 kwa ajili ya wafanyabiashara wa bidhaa ndogo ndogo.
Meneja msimamizi wa soko hilo, Elichilia Mushi
alisema limejengwa kwa mfumo wa kisasa ili kuboresha
huduma za wafanyabiashara hao.
“Tumepanga wafanyabiashara kulingana na aina ya bidhaa
aliyonayo, lengo letu ni kuwavutia watu wengi zaidi na kuboresha huduma ya soko
hili kuwa tofauti na mengine. Pia
tunazingatia suala la usafi,” alisema.
Alisema katika kutekeleza hilo zimewekwa sheria, kanuni na
utarabu ambao utawasaidia kuboresha usafi ndani ya soko hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni