MKUU
wa Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani Abdallah Kihato amewatahadharisha watu
wanaokwenda kununua ardhi katika wilaya yake hasa vijiji vinavyopakana na Ilala
kuwa makini na matapeli wanaovamia maeneo hayo.
Akizungumza
na Blog hii jana ofisini kwake, Kihato alisema kumeibuka malalamiko mengi hasa
katika kijiji cha Tambani kuwepo matapeli wanaovamia mashamba yasiokuwa yao na
kukata viwanja na kuuzia watu kwa madai kuwa eneo hilo liko Ilala.
“Ni
muhimu kwa wanunuzi kufuata taratibu zote za ununuzi wa ardhi kwa
kuwashirikisha viongozi wa kijiji ili kuthibitisha kama muuzaji ni eneo lake,”
alisema kihato.
Alisema
wanazo idara za ardhi kwa kila ngazi na upo utaratibu kwa mnunuzi na muuzaji
kufika ofisi za kijiji kutambuliwa.
“Wakati
mwingine watu wetu wanaingia katika migogoro hiyo kutokana na kuwa na haraka,
wanakosa udadisi hawawezi hata kujiridhisha kwa majirani,” alisema Kihato.
Alisema
wamekubaliana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala kuwa na kikao cha pamoja cha kamati za
ulinzi na usalama kutokana na lawama nyingi za uvamizi kuripotiwa kutokea
maeneo ya Wilaya hiyo.
“Migogoro
mingi imetokana na kuharibiwa kwa ramani ya mwaka 1974 inayoonyesha mipaka ya
wilaya hizi mbili,” alisema.
Alisema
hati nyingi zimeandikwa kuwa kijiji cha Tambani kiko Ilala kitu ambacho si
kweli hakuna mtaa huo katika wilaya hiyo.
Migogoro hiyo ya ardhi katika eneo
hilo imesababisha watu wawili kupoteza maisha yao kutokana na mapigano kati ya
wakazi na jamii ya Wakurya wanaodaiwa kuvamia maeneo ambayo si ya kwao.
mwisho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni