TAASISI ya kijamii ya Rehema Friendship and Solidarity Trust(REFSO) yenye makao yake
Mbezi beach jijini Dar es Salaam imewaondolea kero ya maji iliyokuwa
ikiwakabili wa wakazi wa kijiji cha Tambani, Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani
kwa kuwachimbia kisima kirefu kitakachowasaidia kupata maji bure na karibu.
Akizungumza katika ufunguzi wa kisima
hicho, kiongozi
wa Taasisi ya REFSO, Mirzagha Mehraliyev alisema kuwa wamekuwa wakitoa misaada
mbalimbali kwa jamii ya kitanzania hasa maeneo ya vijijini.
“Tumewafikia
idadi kubwa ya watanzania kwa tukichimba visima virefu vya maji na mpaka sasa
tuna visima 130 Tanzania nzima ambavyo vimeanza kutumika,” alisema Mehraliyev.
Alisema
kisima hicho ambacho kimegharimu kiasi cha tsh.milioni 15 zilizotokana na
wafadhiri kutoka Uturuki.
Alisema
kuwa jamii inayoishi vijijini inakabiliwa na changamoto nyingi mojawapo ni
ukosefu wa maji safi na salama hivyo wao kama watoa misaada wameamuma
kuwasaidia wakazi wa kijiji hicho.
Alisema
mbali na uchimbaji wa visima, REFSO hutoa misaada mbalimbali zikiwemo huduma za
afya, elimu na mambo ya kijamii.
Awali
akisoma risala katika ufunguzi huo, mwakilishi wa kijiji hicho Mmembu Saidi
aliishukuru Taasisi hiyo kwa kuwaondolea kero hiyo ambayo ilikuwa ikiwatatiza
kwa muda mrefu hasa wanawake ambao walitembea umbali mrefu kutafuta maji.
“Pamoja
na kumalizika kwa kero hiyo, kijiji hicho bado kinakabiliwa na changamoto
nyingi za kijamii mojawapo ni ukosefu wa
madaraja yanayowaunganisha na vijiji jirani, zahanati na soko hivyo
msituchoke,” alisema Said.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni