HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam
imesema imedhamilia kulifanya soko la Kisutu kuwa la kisasa kwaajili ya kikudhi
mahitaji ya watumiaji.
Hayo yalielezwa jana na aliyekuwa Mstahiki Meya wa Manispaa
ya Ilala Jerry Silaa wakati alipokuwa akivunja
Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo.
Alisema tayari Manispaa hiyo imesaini mkataba na Benki ya
Rasilimali(TIB) kwaajili ya kujenga soko la kisasa la Kisutu, kwani licha ya
manispaa hiyo kuwa na masoko 18 lakini bado hayoko kwenye ubora unaostahili.
“Manispaa licha ya kuwa na masoko 18 lakini matano t undo
makubwa huku huku kwenye hayo matano kukiwa na hilo la Kisutu ambalo
tumedhamilia liwe la kisasa kwani liko katikati ya Mji, ” alisem Silaa.
Kwa upande mwingine Slaa alisema kuwa Baraza hilo
limevunjwa huku kukiwa na mambo mengi ya kujivunia hususan katika kuandaa
mazingira endelevu ya Uwekezaji.
“Kama Manispaa pia tumefanikiwa kuongeza mapato ya ndani,
Uboreshaji wa Huduma za Kiuchumi, Elimu na Afya, yote hiyo ikiwa ni
kwakushirikiana vizuri na madiwani wote,
” alisema Silaa.
Silaa pia ametangaza adhma yake ya kutaka kugombea nafasi
ya ubunge kwenye jimbo la Ukonga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika
Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
“Ni imani yangu kuwa
mwakani mungu akijaalia nitakuwa nanyi kwenye baraza hili lakini nikiwa kwenye
nafasi nyingine ya Ubunge, kwani kama walivyoniamini wananchi wa kata ya Gongo
la Mboto kuniteua kuwa Diwani wao basi hata kwenye ubunge kazi itakuwanyepesi,”
alisema Slaa.
Mwisho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni