DIWANI wa Kata ya Gongo la Mboto, Jerry Silaa ameainisha
mafanikio aliyoyatekeleza katika kipindi cha miaka mitano tangu achaguliwe kuwa
diwani na Meya wa Manispaa ya Ilala.
Akiainisha mafanikio hayo, alisema kwamba ameweza kutimiza ahadi
mbalimbali alizokuwa ametoa kwa wakazi wa kata za manispaa ya Ilala.
Katika utekelezaji huo, Silaa alivipatia fedha vikundi vya
VICOBA, Genereta, vifaa vya michezo kwa vijana na hati za uthibitisho wa ujenzi
wa barabara zitakazojengwa kwa madiwani.
Silaa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) alitangaza mafanikio hayo katika mkutano wa hadhara jana uliofanyika
katika Shule ya Msingi Kitunda iliyopo Ukonga ambapo pia aliutumia
mkutano huo kutangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CCM katika uchaguzi Mkuu
utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Aidha mafanikio mengine yaliyopatikana wakati wa uongozi
wake, aliyataja kuwa yapo katika sekta ya elimu, afya, maji na ujezi wa
barabara Kata ya Gongolamboto pamoja na kata zote za Manispaa ya Ilala.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni