MFUMUKO
wa bei wa Taifa kwa mwezi juni, 2015 umeongezeka hadi asilimia 6.1 ukilinganisha
na asilimia 5.3 kwa Mei mwaka huu.
Hii
inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka
ulioishia mwezi Juni 2015 ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka
ulioishia Mei 2015.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na
Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo alisema ongezeko hilo limechangiwa na
kuongezeka kwa bei za baadhi ya vyakula na zisizo za vyakula katika kipindi
kilichoishia juni mwaka huu.
Alisema
fahirisi (kipimo) za bei zimeongezeka hadi 158.12 Mei, 2015 kutoka 148.98 juni,
2014.
"Mfumuko
wa bei umeendelea kuongezeka pia kutokana na ongezeko la bei za mafuta hasa petrol kwa
asilimia 5.2 na diesel kwa kwa asilimia 4.5.
"Mfano
mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula kama zilizoonyesha kuongezeka
mwezi juni 2015 zikilinganishwa na bei za juni,2014 ni pamoja na mchele kwa
asilimia 31.5, mahindi kwa asilimia 8.1,unga wa muhogo asilimia 3.7, nyama
asilimia 3.1, samaki asilimia 12.0 na maharage asilimia 11.6. alisema
Kwesigabo.
Kwesigabo
alisema mfumuko wa bei kwa bidhaa zisizo
za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa kwa mfumuko wa bei mwezi juni 2015
zikilinganishwa na bei za juni 2014 na pamoja na bei za mavazi wanaume kwa
asilimia 3.6, mavazi ya wanawake asilimia 2.6,vyakula kwenye migahawa kwa
asilimia 3.5, na huduma za malazi kwa asilimia 3.1.
"Mfumuko
wa bei kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.2 mwezi juni, ukilinganisha
na 0.4 kwa mwezi mei mwaka huu mwaka huu," alisema.
Alisema
uwezo wa shilingi 100 katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 63 na senti
24 mwezi juni, mwaka huu kutoka Septemba, 2010 ikilinganishwa na shilingi 63 na
senti 35 mwezi Mei mwaka huu.
Alisema
hata hivyo mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi za
Afrika Mashariki ambapo kenya umeongezeka kwa asilimia 7.03 kutoka asilimia
6.87 mwezi mei 2015 na Uganda kubaki 4.90 kama ilivyokuwa mwezi mei mwaka huu.
Aidha
amewaomba wananchi kutoa ushirikiano wa dhati kwa ofisi za takwimu za mikoa
wakati wa ukusanyaji wa takwimu mbalimbali kwa lengo la kutoa taarifa zilizo
sahihi kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni