Jumatatu, 22 Juni 2015

TANZANIA KWA UBUNIFU KIBOKO



“TANZANIA ni wabunifu na tunahitaji ubunifu kwa maendeleo ya nchi lakini sio ubunifu huu wa ovyo,” hiyo ni kauli iliyotolewa kwa masikitiko na Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akizungumza na wakuu wa mikoa na wilaya alipokuwa Singida hivi karibuni.
Kauli hii ya Rais ilikuja baada ya baadhi ya watanzania kujaribu kubadilisha matumizi ya vitu kuwa wanavyotaka wao.
 Inawezekana hali ya umaskini wa watu wengi ndio hupelekea baadhi ya watu kubuni njia ambazo zinawasaidia kupata vitu vya gharama nafuu tofauti na uhalisia.
Akiwa Singida Rais anasikitishwa na tabia ya baadhi ya watu wanaotumia vyandarua ambavyo vimegawiwa bure na Serikali kwa kila kaya nchini kwa lengo la kutokomeza malaria na wao kubadilisha lengo lililokusudiwa kwa kufugia kuku ama kuvulia samaki na wengine wakidiriki kujengea msalani.
 “Watu wetu wa ajabu sana, tumegawa vyandarua bure ili sote tuondokane na tatizo la malaria, lakini nasikitika ninavyosikia kuwa wengine wanavitumia kufugia kuku.
“Kweli Tanzania inahitaji ubunifu, lakini siyo ubunifu wa namna hii wa ovyo, tuache kutumia vyandau kufugia kuku, tuvitumie kama ilivyokusudiwa.” Anasema Kikwete.
Vidonge vinavyotibu maradhi mbalimbali
Dawa za kuchochea uchungu kwa wajazito zikiwamo ‘misoprostol’ , ‘oxytocin’ , `Mifecon-Mkit’ zinazopatikana kiholela kwenye maduka ya dawa zimekuwa zikitumika kwa utoaji mimba holela ambao hufanyika bila hofu yoyote.
Vidonge hivyo hupanua shingo ya kizazi na kusababisha hewa kupita kwenye nyumba ya uzazi na kubomoa ukuta wa tumbo la uzazi na kuharibu mimba.
Misoprost -200 maarufu kama ‘miso’ ni vidonge vinavyodaiwa kubadilishwa matumizi yake ya awali na kuwa dawa za kutolea mimba.Jijini Dar es Salaam matumizi ya dawa hii yameongezeka kwa kutolea mimba hasa kwa baadhi ya wanafunzi na wafanyabiashara za ngono.
Dawa ya ‘mkit’ ambalo katika mahojiano na baadhi ya wanafunzi na wafanyabiashara ya ngono wamekuwa walisifia kwa kudai inatoa mimba yenye umri wowote hata pale ‘miso’ inaposhindwa.
 Kwa upande wa dawa ya ‘oxytocin’ watumiaji kuchomwa sindano na kurudi nyumbani kusubiri mimba iharibike.
Tembe nyingine zinazotumiwa ni ‘arzithromycin-500’ ambazo huingizwa sehemu za siri na nyingine humezwa. kazi ya dawa hii si kuharibu mimba bali ni kutibu kama kifua, magonjwa ya zinaa na kukausha vidonda vilivyotokana na kushambuliwa na vimelea.
Dawa hizi hutumika kwa maelekezo yanayotolewa na wahudumu wa maduka ya dawa, wahudumu wa afya wasio na maadili na madaktari ‘vishoka’ mitaani.
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wanakiri kuwa dawa hii inawasaidia lakini wengine walisema si wakati wote kwani wapo waliodai waliitumia lakini badala ya kuharibu iliikomaza mimba.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Elizabeth  Joseph anasema yeye hajawahi kutumia vidonge hivyo lakini rafiki zake hununua kwenye maduka ya dawa na kutumia kutoa mimba.
Matumizi ya dawa ya malaria aina ya Metakelfin yamebadilishwa na sasa ni kutengeneza kipodozi cha kurembesha nywele. Utafiti uliofanywa hivi karibuni na shirika lisilo la kiserikali la Envirocare linalojihusisha na mpango wa  kupunguza madhara yatokanayo na bidhaa za vipodozi kwa binadamu na mazingira, umebaini dawa ya malaria ni aina mojawapo ya kemikali inayotumika kienyeji  katika kutengeneza kipodozi cha kurembesha nywele.

Imeripotiwa kuwa baadhi ya wafugaji wa Mkoa wa Mbeya wanatumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARVs) kwa ajili ya kunenepesha mifugo yao.
Kwa mara ya kwanza habari hizo zililipotiwa na Gazeti hili Toleo Na. 4990  Januari11 , 2010.
 Dawa hizo zinadaiwa kukuza haraka na kunenepesha mifugo kama Nguruwe, ng’ombe, kuku na wengineo.

Inadaiwa kuwa dawa ya kutibu magonjwa ya mifupa indomethacin maarufu kama indocid imekuwa ikitumika kama sumu ya kuulia panya.
“Indocid ni sumu nzuri sana kwa panya, ukiichanganya na chakula panya wakila wanakufa,” anasema Asia Mohammed ambaye ni mkazi wa Uzuri ,Manzese. 
Mbolea za mazao
Baadhi ya wafugaji wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, wanatumia mbolea ya kupandia na kukuzia mazao kulishia mifugo yao kwa madai kuwa huinenepesha. Hayo yalielezwa na Ofisa Tarafa ya Makame, Ibrahim Ole Mario alipokuwa akizungumza katika mafunzo ya wenyeviti 25 wa vikundi vya wakulima wa Kiteto.
Kondom za kike
 Huko Rukwa baadhi ya wanawake mkoani humo wamekuwa wakitumia kondomu za kike kwa kuzivaa kama urembo wa bangili.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj9OCiSiDpKSzRPXc_q_A1pRVVKYOt2xK20xAnA7XJy2Q0aCNWJFJNHWtdKL9pAgaeKyowKLL7lwDtNMYJ6iFoCu3xIXEcjVWTV_n955uzHK1YU1GQQVo3KRgkidaLi_6OMpDYssvxWQsIq/s1600/KINGA.jpg
Matumizi ya sarafu
SARAFU mpya ya shilingi 500 inadaiwa kutumiwa na baadhi ya watu ambao huinunua kwa Sh 2,500 na baadaye kuiyeyusha kwa ajili ya kutengenezea mikufu ya fedha (silver).
Benki kuu ya Tanzania ilitoa ufafanuzi kuhusu uyeyushaji wa sarafu hiyo. Apr 29, 2015 - 500 ni chuma na asilimia 6 ni Nickel, ameeleza Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki katika Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Marcian Kobello.
 “Hakuna kabisa madini ya fedha katika sarafu ya sh. 500,” anasema Bw. Kobello na kuongeza kuwa haitegemewi kwamba mfanyabiashara yeyote anaweza kununua sarafu hiyo kwa bei ya juu kuliko thamani yake halisi.
Maji ya betri pamoja na jik
Jik na maji ya betri yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara kutumiwa kama malighafi na wataalamu wa kutengeneza mikorogo inayotumiwa na baadhi ya wanawake na wanaume kuchubua ngozi za miili yao.
 Utafiti uliofanywa hivi karibuni na shirika lisilo la kiserikali la Envirocare linalojihusisha na mpango wa  kupunguza madhara yatokanayo na bidhaa za vipodozi kwa binadamu na mazingira, umebaini kuwa maji ya betri pamoja na dawa ya kuondoa madoa (jik) vinatumika katika uandaaji wa mikorogo.
Mtafiti kutoka shirika hilo Issa Sen’genge anasema Swali lilikuwa kama kuna vitu vinavyotumika katika kutengeneza mchanganyiko wa kupaka kwenye ngozi au nywele, waliohojiwa walikiri kuchanganya, Metakelfin, Jik, maji ya betri na kemikali nyingine.
 Matumizi hayo ya hatari yanaweza kusababisha madhara makubwa kwa watumiaji.
Watanzania wamekuwa wakibadili matumizi ya vitu mbalimbali hata kama ni hatari kwa afya zao.

Maoni 1 :