KESI
ya madawa ya kulevya yenye thamani ya sh. bilioni 2 inayowakabili watu 13 raia
wa Iran jana imeendelea kupigwa tarehe baada ya upande wa jamhuri kudai kuwa upelelezi
haujakamilika.
Mbele
ya hakimu mkazi wa mahakama ya kisutu Thomas Simba, wakili wa serikali Adolf
Mkini alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea na kwamba anaiomba
mahakama kupanga tarehe nyingine ili kutoa nafasi ya kuendelea na upelelezi.
Hata
hivyo hakimu Simba alimtaka wakili wa serikali kuhakikisha upelelezi
unakamilika au kutoa sababu iwapo atataka tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi
kutokana na kuwa ndio utaratibu mzuri kwani mambo ya kila siku kudai kuwa upelelezi haujakamilika ni mtindo wa
kizamani.
Washitakiwa
katika kesi hiyo ni Mansour Rais, Pohel Mohamed, Rasol Barsh, Gulam Razer, Said
Mohamed, Nazir Pack, Mohamed Rafiq, Rahim Marabzay, Salim Kosal, Vari Mahmoud,
Razer Rais na Allan Javi.
Kesi
hiyo iliahirishwa hadi itakapotajwa tena Juni 29.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni