BAADHI ya wanamuziki wa Bendi ya The African band ‘Twanga
pepeta’ wametishia kuihama bandi hiyo kutokana na kile walichokiita kunyanyaswa
na viongozi wa bendi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa sharti la kutotajwa
majina yao, wanamuziki hao walisema kumekuwepo na manyanyaso katika bendi hiyo
kwa kuwabagua katika kuwalipa mishahara.
“Tumechoshwa na ubaguzi huu maana kwenye kufanya kazi
hatubaguliwi lakini wakati wa kulipwa fedha zetu zinakaa miezi miwili wakati
kuna wenzetu wanalipwa mapema,” alisema mmoja wa wanamuziki hao.
Mwanamuziki mwingine alisema wamekuwa wakitengwa hasa
kipindi cha malipo kwa kuonekana wengine ni bora kuliko wao.
“Kama familia tunazo wote na kila mtu ana majukumu sasa kwa
nini wengine walipwe kwa wakati? Kila mmoja amekuja kutafuta pesa,” alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni