MBUNGE wa Mkuranga Abdallah Ulega(CCM), ameahidi kushughulikia malalamiko ya kukosekana kwa hudumu za afya katika Zahanati ya Mkamba.
Ulega aliahidi hayo wakati akizungumza na Halmashauri Kuu ya Kata ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwashukuru kwa kukisaidia chama hicho kupata ushindi.
Alisema serikali ya CCM ni sikivu anahakika wahudumu watapatikana kwa ajili ya kuboresha huduma hiyo.
Alisema, baada ya kupokea taarifa hiyo anahakikisha anaifikisha katika sehemu husika kwa ajili ya kufanyiwa utekelezaji.
"Nitahakikisha ujumbe unawafikia wizarani kwa ajili kupatiwa wahudumu hao ambao watakuja kuondoa kero hii inayotukabili katika kata hii sitakubali kuona CCM inatiwa masingi kutokana na kushindwa kuwahudumia wananchi,"alisema Ulega.
Aidha Ulega aliahidi kuanza mara moja ujenzi wa barabara ya kutoka Kimanzichana kwenda katika kata hiyo ili kuondoa adha ya usafiri inayowakabili.
"Wazee wangu Mimi na diwani wenu tutafanya kila linalowezekana kutengeneza japo kwa dharura barabara hii ili iweze kutumika tukiwa tunasubiri fungi la serikali," alisema Ulega.

Kwa upande wake mkazi wa kata hiyo, Mikidadi Misomba alimweleza Ulega kuwa akiweza kutatua matatizo manne yanayowàkabili, wao kama wazee wa CCM watatembea kifua mbele.
"Mahitaji yetu ni manne ukitutimizia utakuwa umetuondolea aibu sisi wazee wa CCM ambayo ni kutuboreshea huduma za afya, barabara,maji na kutuondolea wavamizi wenye mifugo ambao wamekuwa wakituharibia mazao na kusababisha njaa," alisema Misomba.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni