KAMPUNI ya Quality Group inayomilikiwa na mfanyabiashara
Yusuf Manji imeondolewa katika jengo iliyokuwa ikilikalia lililoko kiwanja
namba 189/2 barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam kutokana na deni la
malimbikizo ya ya pango la shilingi bilioni 13.
Kampuni hiyo inadaiwa kiasi hicho cha fedha kutokana na
kulimbikiza deni hilo kwa miaka mingi tangu ipangishwe na mmiliki wa jengo hilo
ambaye ni Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Meneja wa Operesheni
wa kampuni ya Udalali ya Yono ambao ndio walipewa zabuni ya kuiondoa kampuni
hiyo, Atukuzwe Muhugo alisema kazi hiyo imefanikiwa baada ya kutoa notisi ya
masaa 24 kuitaka iondoke.
Alisema notisi hiyo iliisha alfajiri ya jana ndipo
walipofika kuiondoa kwa nguvu lakini wafanyakazi walitii sheria na kuanza kutoa
mali zao.
“Wafanyakazi wa Quality Group hawakuwa wajeuli wametii amri
bila shuruti jambo lililoturahisishia kazi yetu,” alisema Atukuzwe.
Alisem jengo hilo litakuwa chini ya Yono mpaka hapo
litakapokabidhiwa kwa PSPF.
Aliyataja ofisi zilizoondolewa kuwa ni Chief Exercutive officer
of Quality Group Company LTD, Gaming Management Ltd, Q Consult Ltd, Quality
Logistics Company Ltd na International Transit Investment Ltd .
Mmoja wa mahusika katika kampuni hiyo ambaye hakutaka
kutaja jina lake alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alisema hajajiandaa kuongea
na wanahabari na hivyo kuwaomba wafike leo saa nane mchana ndipo ataongea.
“I don’t have suit, come tomorrow I will be ready to talk
to you, how could I talk to you without wearing suit? Come tomorrow after lunch
on 2 (siwezi kuzungumza bila kuvaa suti
hivyo nawaomba mje kesho saa nane mchana ),” alisema.
Ilishuhudiwa magari aina ya Isuzu yenye namba za
usajili T385 DAB na T620 DCC yakipakia vitu na kupeleka sehemu ambayo
haikujulikana mara moja.
Uamuzi wa kuindoa Quality Group katika jengo hilo umetokana
na kushindwa katika kesi namba 33 ya mwaka 2009 iliyofungua kampuni hiyo katika mahakama kuu, Divisheni ya ardhi ikipinga
kuondolewa.
Kesi hiyo ilimalizika Novemba 24, mwaka huu kwa mahakama
kumpa haki mmiliki wa jengo hilo PSPF kutafuta dalali wa kumwondoa Quality
Group.
Jaji aliyetoa hukumu hiyo aliamuru kuondolewa kwa Kampuni
hiyo na kuiacha PSPF kama mmiliki wa jengo
hilo na ndipo Yono walipopewa zabuni ya kwenda kumwondoa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni