Jumatatu, 19 Desemba 2016

JELA MIAKA MINNE KWA KUNG'ATA NA KUMEZA SIKIO LA CHACHA

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kwenda jela miaka minne, Chacha  Nyanchini baada ya kupatikana na hatia ya kumng’ata sikio na kulimeza ndugu yake ambaye ni Chacha Kiong’otu maarufu kama Chacha.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi mahakamani hapo na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Adelf Sachore baada ya kujiridhisha na hoja za upande wa mashtaka ambao ulikuwa na mashahidi watano waliotoa ushahidi pasi na kuacha shaka.
“Ninakuhukumu kutumikia kifungo cha miaka minne baada ya kupatikana na hatia ya kumng’ata sikio la kutosha na kukimeza kipande cha sikio cha mlalamikaji huku ukijua fika kuwa kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa taratibu za nchi,” alisema Sachore.
Awali kabla ya hukumu hiyo kutolewa wakili wa Serikali, Chesence Gavyole alidai kuwa hakukuwa nakumbu kumbu za mashtaka ya nyuma dhidi ya mshtakiwa na hivyo kuiomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wote wenye tabia kama hizo za kung’ata wenzao.
Katika utetezi wake juu ya kwanini mahakama isimpatie adhabu kali, Nyanchini alidsai kuwa anafamilia inayomtegemea na kwamba hakukusudia kufanya hivyo, hivyo mahakama imsamehe kwa kuwa lilikuwa ni kosa lake la kwanza utetezi ambao ulitupiliwa mbali.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka ilidaiwa kuwa Februari 12, mwaka huu katika eneo la Kivule Majohe ndani ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam alimng’ata na meno sikio la kushoto la mlalamikaji na kukimeza kipande hicho kwa kile kilichodaiw akuwa kuwa ni ugomvi wa kifamilia.

Mwisho 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni