CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema Makaburu walimrubuni Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wakati huo, William
Kusila, akasaini mkataba kati ya mikataba ya Alliance Air kwenye karatasi ikiwa
na nembo ya wizara bila ya maandishi yoyote na kuwapatia makaburu waende
wakajaze maelezo wanayoyataka nchini kwao jambo lililochangia kuitesa Air
Tanzania hadi leo.
hayo yalisema jana na Mwenyekiti wa
Chama hicho, Anna MghwiraAnna alipozungumza na waandishi wa habari ambapo alisema miaka ya 1990 viongozi wa Wizara ya Mawasiliano
na Uchukuzi kupitia kitendo cha usafiri wa anga waliuza njia(Routes) za ATCL
kwa mashirika mengine ya ndege na kuilazimisha ATCL kuingia katika mikataba
mibovu ya ushirikiano na kulifilisi
shilika hilo.
“Kwa ujanja kampuni ya Swissport ilianzishwa ikiwa chini ya
mkurugenzi wake Esther Maro ambaye alikuwa ni mdogo wake Anna Mkapa, na
kulinyang’anya shirika majukumu yake huku Gulf Air, Emirates na Kenya Airways
zikiongezewa njia na wakawa waendeshaji wa njia kama mashirika ya Taifa la
Tanzania,” alisema Anna.
Alisema katika awamu ya tatu na nne ATC ilinyang’anywa
huduma za chini uwanjani na kulazimishwa kuingia ubia na South African
Airways(SAA) na Makaburu hao kuilazimisha menejimenti na bodi ya ATC kupunguza
marubani15 na wahandisi 30 kwa kuwadanganya kuuza ndege za kizamani.
“Ndege zilizouzwa aina ya B737-200 zilikuwa zinaruka vizuri
kwa safari za ndani na nje zilifika Ulaya, Marekani na Afrka kusini, ambazo
zilituwa na makampuni mengi kwa ahadi ya kutuletea za kisasa zenye uwezo wa
kusafiri umbali mrefu,” alisema Anna.
aidha kimeishauri serikali kulirudishia
Shirika la Ndege la Taifa(ATCL) mamlaka ya kumiliki huduma zote za chini(Ground
handling) za uendeshaji wa viwanja vya ndege.
Pia wameiomba serikiali kuunda kitengo cha uwezeshaji ambacho
kitahudumia shughuli zote zinazofanyika katika viwanja vya ndege nchini ili
kuimarisha usalama wa nchi.
alisema huduma hizo ni pamoja na huduma kwa abiria,
kuhudumia mizigo yote ya Ndege, huduma za vyakula na kambi ndani ya ndege na
ukatishaji wa tiketi.
Alisema huduma hizo ni moja ya vitega uchumi muhimu katika
mashirika ya ndege ya nchi, Duniani kote kwa kuwa biashara ya ndege haitegemei
kuwa na ndege pekee hivyo kutaka maandalizi yaanze mapema ili zikiwasili mfumo
wa uzalishaji uko vizuri.
“Kwa kutoa huduma hizi kwa umakini na kuvimilikisha viwanja
kwa wananchi wazalendo ambao watakuwa waajiriwa wake, shirika litaweza
kuzalisha fedha nyingi na kutoa ajira kwa watanzania,” alisema Anna.
Alisema kwa muda mrefu sasa Tanzania imekwenda kinyume na
utaratibu huo jambo ambalo ni kuinyakulia ATCL raslimali zake na hivyo kuinyima
mapato.
Alisema ubinafsishaji wa raslimali hizo haukufanyika kwa
lengo la kuimarisha usimamizi bali ulichangiwa na tabia ya rushwa ya kupata
asilimia kumi ya faida kwa viongozi walioongoza na kulididimiza taifa.
“Uendeshaji wa mifumo ya compyuta,mfumo wa usalama wa
viwanja, utunzaji wa mizigo, utunzaji wa abiria, kitengo cha uhandisi na huduma
ya kuuza mafuta ya ndege viwe chini ya shirika kwa ajili ya usalama wa nchi na
kuzalisha ajira, kwani ni rahisi kwa
wageni kurubuniwa” alisema Anna.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni