MGOGORO
wa ardhi unaohusisha vijiji vinne vya Wilaya ya Mkuranga umechukua sura mpya
baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Filberto Sanga kuwataka wakazi wa vijiji hivyo kukaa vikao
vya kutayarisha mihutasari kumwomba Rais kufuta hati ya shamba ambalo limekuwa
likitumiwa na wananchi kwa muda mrefu.
Mgogoro huo wa eneo la ekari 2472 unahusisha vijiji
vinne vya kata mbili ya Tambani na Mipeko vyenye wakazi takribani 45,000
wakiwamo Rais Mstaafu Ali Hassani Mwinyi,
Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Warioba, Jaji Hamis Msumi, Rashidi Kawawa wakihusishwa kuvamia eneo la Kareem Manji na
Entias Rajuani.
Sanga aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara kati
ya wananchi na kamati ya usalama ya wilaya hiyo uliokuwa na lengo la kujadili
shamba hilo linaloonekana kutishia usalama wa raia pamoja na mali zao.
Alisema viongozi wa vijiji hivyo wanapaswa kuhakikisha
shughuli zote za upimaji ardhi katika vijiji hivyo vilivyodaiwa kumilikiwa na
wamiliki hao zinasitishwa mpaka pale taratibu mbalimbali zitakapokamilishwa.
Alisema viongozi wa vijiji hivyo wanapaswa kuhakikisha hakuna mtu yeyote anayeweza kufanya maamuzi ya aina yoyote katika vijiji hivyo pasipo kupata ruhusa na kibali kutoka katika ofisi za Serikali.
“Anzeni vikao
kujadili suala hili na kuandika muhtasari kwa ngazi za juu kuomba kufutwa
umiliki wa shamba hili,” alisema Sanga.
Sanga aliwahakikishia wananchi wa eneo hilo kuwa wako
katika mikono salama kuwa hakuna atakayewaondoa katika eneo hilo bila kufuata
sheria.
“Mimi mkuu wa wilaya sina ardhi ya kuwaweka watu 45,000
wanaoondolewa hapa hivyo wakija waambieni waanzie kwangu… kwani kuwagusa
wananchi bila kupitia viongozi huo ni uhuni,” ali
sema.
Aliwatahadhalisha wananchi kutouza holela ardhi jambo ambao
husababisha migogoro kuwa mingi.
“Acheni kuuza ardhi, niwaombe wenyeviti wasaidieni wananchi
wasiuze ardhi, na kama mtu anauza eneo lake uuzaji huo ufanyike hadharani kwa
yeye na mnunuzi kusimama mbele ya wananchi ili mgogoro ukitokea wao ndio wawe
wa kwanza kusuluhisha,” alisema Sanga.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo,Mhandisi Ally
Munde
Naye mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega amemuomba
Rais Dk. John Magufuli kufuta hatimiliki ya shamba hilo baada ya wawekezaji hao
kushindwa kuliendeleza kwa zaidi ya miaka 50 na badala yake wapewe wananchi.
Alisema shamba hilo lilitelekezwa kwa kipindi kirefu
na wawekezaji hao, hali iliyopelekea wakazi wa kata ya Tambani pamoja na Mipeko
kuyaendeleza kwa kufanya ujenzi na shughuli mbalimbali za maendeleo.
Ulega alisema Wakazi wa maeneo hayo waliweza
kutafuta hati miliki ya maeneo waliyokuwa wanamiliki kwa kipindi chote na
kushangazwa na kitendo cha wamiliki hao kuwataka kutoka katika maeneo yao kwa
madai kuwa wamevamia eneo hilo.
Alisema wananchi wa vijiji vya Mlamleni, Luzando, Mwanambaya pamoja na Mipeko
wamekuwa katika hali ya taharuki toka walipopewa notisi ya siku 21 ya kuwataka
waondoke katika maeneo hayo ambayo wameyaendeleza kwa shughuli mbalimbali za
kimaendeleo.
"Mi najua Rais wetu ni msikivu na anaweza
kuzifanyia kazi kero za wananchi kwa wakati, na kero hii naamini atatilia mkazo
kwa sababu wameshindwa kufanya shughuli za maendeleo kwa sasa kwa sababu ya
watu wawili ,” alisema Ulega.
Hata hivyo Ulega alimueleza Mkuu wa Wilaya ya
Mkuranga kumuagiza Ofisa Ardhi Mteule
alimweleza
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kutoruhusu kampuni ya 'Ardhi Plan' kupima maeneo
ya wilaya hiyo kwani kama ataruhusu kampuni hiyo kufanya upimaji watapelekea
kutokea kwa vurugu ambazo zinaweza kusababisha hali ya amani na utulivu
kutokuwepo katika wilaya hiyo.
Naye Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega ambaye pia
ni muhanga alisema walikubwa na taharuki baada ya kupokea notisi ya siku 21
ikiwataka kuondoka katika eneo hilo.
“Tutafuata taratibu na sheria kufikisha kilio chetu kwa
rais kumwomba alifutite shamba hilo kwa kuwa alishindwa kuliendeleza kwa muda
wa zaidi ya miaka 50,” alisema Ulega.
Alimwomba DC kumwagiza Ofisa Ardhi mteule kumpa mmiliki
huyo notisi ya siku 90 ya kusudio la kulifuta shamba hilo.
“Hakuna shamba hapa, ninaona nyumba za watu tu, hivi mimi
DC mstaafu nitapata wapi tena fedha za kununua kiwanja,” alisema Ulega.
Akisimulia historia ya shamba hilo la Luzando, Diwani wa kata ya Tambani, Ally Mtamilwa alisema shamba hilo lenye hati namba 1281 lilimilikiwa na kampuni ya Mzungu iliyoitwa Seneda aliyekuwa akilima mkonge kabla ya kuhamishiwa kwa Akibaru February,1952.
Akisimulia historia ya shamba hilo la Luzando, Diwani wa kata ya Tambani, Ally Mtamilwa alisema shamba hilo lenye hati namba 1281 lilimilikiwa na kampuni ya Mzungu iliyoitwa Seneda aliyekuwa akilima mkonge kabla ya kuhamishiwa kwa Akibaru February,1952.
“Mwaka 1978 Waziri Mkuu wa wakati huo hayati, Edward
Sokoine alitangaza vijiji vya nguvu kazi vikiwamo Mwanadilatu, Gezaulole,Tegeta
na katika shamba hilo ili walima kipindi hicho Akibaru aliondoka muda mrefu,”
alisema Mtamilwa.
Alisema baada ya watu hao kupelekwa katika mashamba ya
nguvu kazi waliendelea kuishi hapo kabla ya wanaodaiwa kuwa ni wajukuu wa
Akibaru ambao ni Manji na Rajuani kufika katika eneo hilo kwa madai ya kutaka
kuliendeleza wakiwa na hati ya mwaka 1952.
“Baada ya kukuta wananchi wakiendelea na kilimo waliridhia
kutoa ekari 1472 kwa wananchi na wao kubakiwa na ekari 1,000 ambapo mwaka 1990
walifanya tathmini ya kuwaondoa wananchi waliokuwa ndani ya ekari walizobakiza
na waliondoka bila kuwalipa,” alisema Mtamilwa.
Mtamilwa alisema Manji na mwenzake walituma kampuni ya
upimaji wa ardhi iitwayo Ardhi Plan kupima viwanja katika eneo hilo.
“Waliwataka wenye maeneo ambayo hayajajengwa kulipwa kila
ekari shilingi milioni moja na waliojenga kupimiwa viwanja na kulipa gharama za
upimaji,” alisema Mtamilwa.
Aliongeza kuwa baada ya wananchi kutokuafiki suala hilo
ndipo Manji na mwenzake kupitia mwanasheria wao waliandika notisi ya siku 21
kuwataka wakazi hao kuondoka kabla ya Disemba 19, 2016.
mwisho