Jumatatu, 6 Julai 2015

SILAA AELEZA MAFANIKIO YAKE UKONGA


DIWANI wa Kata ya Gongo la Mboto, Jerry Silaa ameainisha mafanikio aliyoyatekeleza katika kipindi cha miaka mitano tangu achaguliwe kuwa diwani na Meya wa Manispaa ya Ilala.
Akiainisha mafanikio hayo, alisema kwamba ameweza kutimiza ahadi mbalimbali alizokuwa ametoa kwa wakazi wa kata za manispaa ya Ilala.
Katika utekelezaji huo, Silaa alivipatia fedha vikundi vya VICOBA, Genereta, vifaa vya michezo kwa vijana na hati za uthibitisho wa ujenzi wa barabara  zitakazojengwa kwa madiwani.
Silaa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alitangaza mafanikio hayo katika mkutano wa hadhara jana uliofanyika katika Shule ya Msingi Kitunda iliyopo Ukonga   ambapo pia aliutumia mkutano huo kutangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CCM katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu. 
Aidha mafanikio mengine yaliyopatikana wakati wa uongozi wake, aliyataja kuwa yapo katika sekta ya elimu, afya, maji na ujezi wa barabara Kata  ya Gongolamboto pamoja na kata zote za Manispaa ya Ilala.

SOKO LA KISUTU KUWA LA KISASA ZAIDI



HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam imesema imedhamilia kulifanya soko la Kisutu kuwa la kisasa kwaajili ya kikudhi mahitaji ya watumiaji.
Hayo yalielezwa jana na aliyekuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wakati alipokuwa akivunja  Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo.
Alisema tayari Manispaa hiyo imesaini mkataba na Benki ya Rasilimali(TIB) kwaajili ya kujenga soko la kisasa la Kisutu, kwani licha ya manispaa hiyo kuwa na masoko 18 lakini bado hayoko kwenye ubora unaostahili.
“Manispaa licha ya kuwa na masoko 18 lakini matano t undo makubwa huku huku kwenye hayo matano kukiwa na hilo la Kisutu ambalo tumedhamilia liwe la kisasa kwani liko katikati ya Mji, ” alisem Silaa.
Kwa upande mwingine Slaa alisema kuwa Baraza hilo limevunjwa huku kukiwa na mambo mengi ya kujivunia hususan katika kuandaa mazingira endelevu ya Uwekezaji.
“Kama Manispaa pia tumefanikiwa kuongeza mapato ya ndani, Uboreshaji wa Huduma za Kiuchumi, Elimu na Afya, yote hiyo ikiwa ni kwakushirikiana vizuri na madiwani wote,  ” alisema Silaa.
Silaa pia ametangaza adhma yake ya kutaka kugombea nafasi ya ubunge kwenye jimbo la Ukonga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
 “Ni imani yangu kuwa mwakani mungu akijaalia nitakuwa nanyi kwenye baraza hili lakini nikiwa kwenye nafasi nyingine ya Ubunge, kwani kama walivyoniamini wananchi wa kata ya Gongo la Mboto kuniteua kuwa Diwani wao basi hata kwenye ubunge kazi itakuwanyepesi,” alisema Slaa.
Mwisho                               


HUKUMU YA MBASHA YAPIGWA KALENDA



MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala Juni 13, mwaka huu itaeleza iwapo mwimbaji na mfanyabiasha Emmanuel Mbasha ana kesi ya kujibu au la.
Mwendesha Mashtaka Munde Kalombora alisema kwamba mahakama itaeleza baada ya kupitia hoja za pande zote mbili.
Mbasha ambaye ni Mume wa mwimbaji maarufu wa muziki wa injili nchini, Flora mbasha anakabiliwa na tuhuma za ubakaji.
Kesi hiyo inasikilizwa mahakamani hapo na hakimu Flora Mjaya na mwendesha mashtaka Munde kalombora.
"Mara ya mwisho tarehe ilipangwa Julai 4 kimakosa kwani siku hiyo ni jumamosi, leo ( jana) mbasha alikuja isipokuwa mawakili wake, ndio maana Hakimu amepanga waje Julai 13, ili iamuliwe", alisema Munde.
katika kesi hiyo Mbasha anadaiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni shemeji yake.

REFSO WASAIDIA KISIMA TAMBANI



TAASISI ya kijamii ya Rehema Friendship  and Solidarity Trust(REFSO) yenye makao yake Mbezi beach jijini Dar es Salaam imewaondolea kero ya maji iliyokuwa ikiwakabili wa wakazi wa kijiji cha Tambani, Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani kwa kuwachimbia kisima kirefu kitakachowasaidia kupata maji bure na karibu.
Akizungumza katika ufunguzi wa kisima hicho, kiongozi wa Taasisi ya REFSO, Mirzagha Mehraliyev alisema kuwa wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali kwa jamii ya kitanzania hasa maeneo ya vijijini.
“Tumewafikia idadi kubwa ya watanzania kwa tukichimba visima virefu vya maji na mpaka sasa tuna visima 130 Tanzania nzima ambavyo vimeanza kutumika,” alisema Mehraliyev.
Alisema kisima hicho ambacho kimegharimu kiasi cha tsh.milioni 15 zilizotokana na wafadhiri kutoka Uturuki.
Alisema kuwa jamii inayoishi vijijini inakabiliwa na changamoto nyingi mojawapo ni ukosefu wa maji safi na salama hivyo wao kama watoa misaada wameamuma kuwasaidia wakazi wa kijiji hicho.
Alisema mbali na uchimbaji wa visima, REFSO hutoa misaada mbalimbali zikiwemo huduma za afya, elimu na mambo ya kijamii.
Awali akisoma risala katika ufunguzi huo, mwakilishi wa kijiji hicho Mmembu Saidi aliishukuru Taasisi hiyo kwa kuwaondolea kero hiyo ambayo ilikuwa ikiwatatiza kwa muda mrefu hasa wanawake ambao walitembea umbali mrefu kutafuta maji.
“Pamoja na kumalizika kwa kero hiyo, kijiji hicho bado kinakabiliwa na changamoto nyingi za kijamii mojawapo ni ukosefu wa  madaraja yanayowaunganisha na vijiji jirani, zahanati na soko hivyo msituchoke,” alisema Said.

DIWANI WA MBAGALA AAGA RASMI



DIWANI wa kata ya Mbagala, Manispaa ya Temeke,jijini Dar es Salaam,Aggrey Kayombo amewataka viongozi wa dini kufundisha maadili ya kitanzania hasa kwa vijana ambao kwa sasa wanakumbwa na wimbi la utandawazi na kupoteza asili yao.
Kayombo aliyasema hayo juzi katika msikiti wa Salama uliopo kizuiani Mbagala wakati akizungumza na viongozi wa Bakwata wa kata hiyo katika hafla fupi ya kuwaaga na kuwashukuru kwa ushirikiano waliouonyesha katika kipindi cha uongozi wake.
“Viongozi wa dini mna nafasi kubwa katika kutoa elimu ya maadili kwa vijana na watoto ili waweze kuwa na tabia njema na kioo cha taifa la kesho hivyo basi timizeni wajibu huu, ” alisema Kayombo.
Alisema kuwa walimu wa dini wana nafasi kubwa kuliko viongozi wa siasa katika ulinzi wa amaani na utulivu kutokana na mafundisho yao ya kumjua Mungu na kutambuana wenyewe ambayo huleta hofu ya Mungu na hivyo kuleta amani ya nchi.
Aidha aliwaomba kuwapa ushirikiano wale wote wanaoomba kugombea uongozi kwa ngazi mbalimbali kwani  wako sahihi kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi.
“Wazee wangu nawaomba ushirikiano mlionipa mimi mpeni yeyote atakaechaguliwa kuwa kiongozi katika nafasi  yoyote  hii ndio demokrasia,” alisema Kayombo.
Awali akisoma risala kwa niaba ya viongozi hao, katibu wa Bakwata wa kata ya Mbagala, Saidi Msati alisema Diwani huyo aliweza kuwaunganisha viongozi wa dini mbalimbali ndani ya kata hiyo na kuleta mshikamano, umoja na amani ambayo imedumu muda wote alipokuwepo madarakani.

                                 

Jumatatu, 22 Juni 2015

TANZANIA KWA UBUNIFU KIBOKO



“TANZANIA ni wabunifu na tunahitaji ubunifu kwa maendeleo ya nchi lakini sio ubunifu huu wa ovyo,” hiyo ni kauli iliyotolewa kwa masikitiko na Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akizungumza na wakuu wa mikoa na wilaya alipokuwa Singida hivi karibuni.
Kauli hii ya Rais ilikuja baada ya baadhi ya watanzania kujaribu kubadilisha matumizi ya vitu kuwa wanavyotaka wao.
 Inawezekana hali ya umaskini wa watu wengi ndio hupelekea baadhi ya watu kubuni njia ambazo zinawasaidia kupata vitu vya gharama nafuu tofauti na uhalisia.
Akiwa Singida Rais anasikitishwa na tabia ya baadhi ya watu wanaotumia vyandarua ambavyo vimegawiwa bure na Serikali kwa kila kaya nchini kwa lengo la kutokomeza malaria na wao kubadilisha lengo lililokusudiwa kwa kufugia kuku ama kuvulia samaki na wengine wakidiriki kujengea msalani.
 “Watu wetu wa ajabu sana, tumegawa vyandarua bure ili sote tuondokane na tatizo la malaria, lakini nasikitika ninavyosikia kuwa wengine wanavitumia kufugia kuku.
“Kweli Tanzania inahitaji ubunifu, lakini siyo ubunifu wa namna hii wa ovyo, tuache kutumia vyandau kufugia kuku, tuvitumie kama ilivyokusudiwa.” Anasema Kikwete.
Vidonge vinavyotibu maradhi mbalimbali
Dawa za kuchochea uchungu kwa wajazito zikiwamo ‘misoprostol’ , ‘oxytocin’ , `Mifecon-Mkit’ zinazopatikana kiholela kwenye maduka ya dawa zimekuwa zikitumika kwa utoaji mimba holela ambao hufanyika bila hofu yoyote.
Vidonge hivyo hupanua shingo ya kizazi na kusababisha hewa kupita kwenye nyumba ya uzazi na kubomoa ukuta wa tumbo la uzazi na kuharibu mimba.
Misoprost -200 maarufu kama ‘miso’ ni vidonge vinavyodaiwa kubadilishwa matumizi yake ya awali na kuwa dawa za kutolea mimba.Jijini Dar es Salaam matumizi ya dawa hii yameongezeka kwa kutolea mimba hasa kwa baadhi ya wanafunzi na wafanyabiashara za ngono.
Dawa ya ‘mkit’ ambalo katika mahojiano na baadhi ya wanafunzi na wafanyabiashara ya ngono wamekuwa walisifia kwa kudai inatoa mimba yenye umri wowote hata pale ‘miso’ inaposhindwa.
 Kwa upande wa dawa ya ‘oxytocin’ watumiaji kuchomwa sindano na kurudi nyumbani kusubiri mimba iharibike.
Tembe nyingine zinazotumiwa ni ‘arzithromycin-500’ ambazo huingizwa sehemu za siri na nyingine humezwa. kazi ya dawa hii si kuharibu mimba bali ni kutibu kama kifua, magonjwa ya zinaa na kukausha vidonda vilivyotokana na kushambuliwa na vimelea.
Dawa hizi hutumika kwa maelekezo yanayotolewa na wahudumu wa maduka ya dawa, wahudumu wa afya wasio na maadili na madaktari ‘vishoka’ mitaani.
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wanakiri kuwa dawa hii inawasaidia lakini wengine walisema si wakati wote kwani wapo waliodai waliitumia lakini badala ya kuharibu iliikomaza mimba.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Elizabeth  Joseph anasema yeye hajawahi kutumia vidonge hivyo lakini rafiki zake hununua kwenye maduka ya dawa na kutumia kutoa mimba.
Matumizi ya dawa ya malaria aina ya Metakelfin yamebadilishwa na sasa ni kutengeneza kipodozi cha kurembesha nywele. Utafiti uliofanywa hivi karibuni na shirika lisilo la kiserikali la Envirocare linalojihusisha na mpango wa  kupunguza madhara yatokanayo na bidhaa za vipodozi kwa binadamu na mazingira, umebaini dawa ya malaria ni aina mojawapo ya kemikali inayotumika kienyeji  katika kutengeneza kipodozi cha kurembesha nywele.

Imeripotiwa kuwa baadhi ya wafugaji wa Mkoa wa Mbeya wanatumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARVs) kwa ajili ya kunenepesha mifugo yao.
Kwa mara ya kwanza habari hizo zililipotiwa na Gazeti hili Toleo Na. 4990  Januari11 , 2010.
 Dawa hizo zinadaiwa kukuza haraka na kunenepesha mifugo kama Nguruwe, ng’ombe, kuku na wengineo.

Inadaiwa kuwa dawa ya kutibu magonjwa ya mifupa indomethacin maarufu kama indocid imekuwa ikitumika kama sumu ya kuulia panya.
“Indocid ni sumu nzuri sana kwa panya, ukiichanganya na chakula panya wakila wanakufa,” anasema Asia Mohammed ambaye ni mkazi wa Uzuri ,Manzese. 
Mbolea za mazao
Baadhi ya wafugaji wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, wanatumia mbolea ya kupandia na kukuzia mazao kulishia mifugo yao kwa madai kuwa huinenepesha. Hayo yalielezwa na Ofisa Tarafa ya Makame, Ibrahim Ole Mario alipokuwa akizungumza katika mafunzo ya wenyeviti 25 wa vikundi vya wakulima wa Kiteto.
Kondom za kike
 Huko Rukwa baadhi ya wanawake mkoani humo wamekuwa wakitumia kondomu za kike kwa kuzivaa kama urembo wa bangili.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj9OCiSiDpKSzRPXc_q_A1pRVVKYOt2xK20xAnA7XJy2Q0aCNWJFJNHWtdKL9pAgaeKyowKLL7lwDtNMYJ6iFoCu3xIXEcjVWTV_n955uzHK1YU1GQQVo3KRgkidaLi_6OMpDYssvxWQsIq/s1600/KINGA.jpg
Matumizi ya sarafu
SARAFU mpya ya shilingi 500 inadaiwa kutumiwa na baadhi ya watu ambao huinunua kwa Sh 2,500 na baadaye kuiyeyusha kwa ajili ya kutengenezea mikufu ya fedha (silver).
Benki kuu ya Tanzania ilitoa ufafanuzi kuhusu uyeyushaji wa sarafu hiyo. Apr 29, 2015 - 500 ni chuma na asilimia 6 ni Nickel, ameeleza Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki katika Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Marcian Kobello.
 “Hakuna kabisa madini ya fedha katika sarafu ya sh. 500,” anasema Bw. Kobello na kuongeza kuwa haitegemewi kwamba mfanyabiashara yeyote anaweza kununua sarafu hiyo kwa bei ya juu kuliko thamani yake halisi.
Maji ya betri pamoja na jik
Jik na maji ya betri yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara kutumiwa kama malighafi na wataalamu wa kutengeneza mikorogo inayotumiwa na baadhi ya wanawake na wanaume kuchubua ngozi za miili yao.
 Utafiti uliofanywa hivi karibuni na shirika lisilo la kiserikali la Envirocare linalojihusisha na mpango wa  kupunguza madhara yatokanayo na bidhaa za vipodozi kwa binadamu na mazingira, umebaini kuwa maji ya betri pamoja na dawa ya kuondoa madoa (jik) vinatumika katika uandaaji wa mikorogo.
Mtafiti kutoka shirika hilo Issa Sen’genge anasema Swali lilikuwa kama kuna vitu vinavyotumika katika kutengeneza mchanganyiko wa kupaka kwenye ngozi au nywele, waliohojiwa walikiri kuchanganya, Metakelfin, Jik, maji ya betri na kemikali nyingine.
 Matumizi hayo ya hatari yanaweza kusababisha madhara makubwa kwa watumiaji.
Watanzania wamekuwa wakibadili matumizi ya vitu mbalimbali hata kama ni hatari kwa afya zao.