MKUU wa Wilaya ya Kigamboni, Hashimu Mgandilwa amewataka
wananchi wa Dar es Salaam kuondoa dhana kuwa Fukwe zote za wilaya hiyo ni za
kulipia.
Akizungumza muda mfupi baada ya kufanya usafi katika
maeneo ya fukwe, Mgandilwa alisema eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi ni mali ya umma hivyo wasiogope kwenda
kutembelea.
Alisema kwa mujibu wa sheria eneo lililopo ndani ya mita 60
kutoka kingo za bahari ni mali ya umma na hakuna mwenye mamlaka nayo isipokuwa
serikali.
“Changamoto iliyopo hapa ni ukosefu wa njia za kuingilia
ambapo kwa sasa kuna njia zipo wazi na nitakutana na wizara ya Maliasili na
Utalii kuangalia namna ya kuweka njia zaidi za wananchi kuingia,” alisema
Mgandilwa.
Aidha amewakikishia usalama wananchi na wageni
watakaokwenda kutembelea katika fukwe hizo.
“Tumefanya usafi kama kuhamasisha utalii wa ndani na nje
katika eneo hili kwa kuwa sasa ni sehemu ya utalii wa jiji la Dar es Salaam,”
alisema Mgandilwa.
Mgandilwa alivitaja vivutio mbalimbali vilivyopo katika
wilaya hiyo kuwa ni mbuyu wenye umbo la chupa ya shampeni, visiwa sita kikiwamo
cha Sinda chenye mazalia ya kasa, jengo kale lililojengwa na Wajerumani.
Aliwashukuru wanamuziki waliotoka nje na ndani ya nchi
kushiriki usafi na kuhamasisha utalii wa Kigamboni.
“Uwepo wenu hapa
utaihamasisha jamii na kuitangaza Tanzania kim,ataifa,” alisema.
Naye mwanamuziki wa miondoko ya kufokafoka kutoka
Marekani,Akua Naru alisema amefarijika kushiriki usafi wa fukwe na kuchangia
kutoa elimu ya utalii kwa watanzania.
“Tutaitangaza vema nchi hii kwa kuwa na fukwe nzuri na
utulivu mkubwa hasa kwa sisi wasanii kufanya shughuli zetu,” alisema Akua.
Naye Fred Maliki(Mkoloni) kutoka katika kundi la wagosi wa
Kaya alisema amefurahi kuanza mwaka akiwa na jamii.
“Kushiriki kufanya usafi kwa vijana ina maana tunajitambua
na tunaweza kuhasisha utalii kwa Wilayah ii,” alisema Mkoloni.
mwisho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni