Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simoni Sirro alisema baada ya kufanya tukio hilo la wizi katika eneo la Tazara, majambazi hao waliokuwa wanne, walipanga kwenda kufanya tukio lingine katika jengo la White House Tower lililopo Mikocheni.
“Tukio hilo lilitokea jana(juzi),kwenye muda wa saa 5:20, eneo la Mikocheni kwenye jengo la kibiashara la White Star Tower, tulipata taarifa kuna
hao majambazi ambao waliofanya tukio
kwenye barabara ya Nyerere na kuchukua milioni 25,naamini walinogewa na hizo
fedha wakaenda tena kufanya ujambazi.
“Baada ya kupata taarifa hiyo mapema,vijana wetu
wakaenda kujipanga na walipoingia,askari wakapiga risasi ili majambazi
wajisalimishe lakini nao walijibu, ndipo majibizano yalipoanza na kuwauwa watatu na kukamata bastola moja aina
ya SIG SAUER yenye namba P 229 ikiwa na risasi nne ndani ya magazine,”alisema
Kamishna Sirro.
Alisema mmoja wa majambazi hao alifanikiwa kutoroka kwa kutumia usafiri wa pikipiki na jeshi hilo linaendelea kumtafuta.
Kamishna Sirro alisema wataendelea kupambana na suala la
unyanganyi wa kutumia silaha katika jiji
la Dar es Salaam.
Katika tukio lingine,Kamishna Sirro alisema
wanamshikilia mkazi wa Tundwi Songani,kata ya Pemba Mnazi,Wilaya ya Kigamboni, Anwaz
Ally kwa kukuta na bastola moja aina ya BARRETA ikiwa na risasi 23.
Alisema silaha hiyo ilipatikana baada ya kupekuliwa
maungoni na kumkuta nayo ikiwa imefutwa namba huku akiwa hana kibali halali cha
umiliki wa silaha hiyo.
“Mtuhumiwa huyo alipekuliwa katika chumba chake
anachoishi ambapo alikutwa na risasi 23 za silaha ya BARRETA aliyokuwa
ameificha ndani ya soksi.
“Mahojiano yanaendelea ili kubaini matumizi
ya silaha hiyo, kwani kuna taarifa za kutumika kwa silaha hiyo kwenye matukio
ya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam,”alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni