MKUU wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga amewaonya wanaume
wenye tabia ya kufanya mapenzi na wanafunzi kuwa hawatasalimika na mkono wa
sheria.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa wananchi katika
kata ya Mipeko, Sanga alisema wanaume wenye tabia hizo kama hawatabadilika
wataishia magerezani.
“Nyinyi wanaume acheni kutamani wanafunzi na muwaogope sana
maana sheria haitawaacha salama,” alisema.
Alisema katika mwaka huu anawaomba watoto wote wanaotakiwa
kwenda shule wapelekwe ili kukinusuru na ujinga kizazi hicho.
“Watoto wanaotakiwa kwenda darasa la kwanza waende na
waliofaulu kwenda kidato cha kwanza waende atakayeshindwa kumpeleka mwanaye
shule hatua kali za sheria dhidi yake zitachukuliwa,” alisema Sanga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni