IDADI ya
majengokale katika jiji la Dar es Salaam yanahofiwa kupotea kutokana kukua kwa
kasi kwa jiji hilo.
Akizungumza
katika kongamano la urithi na uhifadhi wa majengo kale, Mkurugenzi wa Kituo cha
Urithi na ubunifu Majengo Dar es Salaam, Aida Mulokozi alisema mpaka sasa
majengokale yanayotambuliwa na serikali ni 25 tu.
Alisema sura
ya jiji hilo imebadilika kutokana na ukuaji wa kasi hivyo kutishia urithi wa
kihistoria wa majengokale.
“Leo Dar es
Salaam ni miongoni mwa majiji kumi yanayokuwa kwa haraka zaidi Duniani kutokana
na shinikizo la uchumi maslahi ambayo yanayogongana na mamlaka dhaifu hivyo urithi
wake uko katika hatari ya kupotea.
“Kasi ya
maendeleo ni kubwa na kubasababisha mabadiliko ya haraka huku majengo mengi ya
kihistoria kuvunjwa,” alisema Aida.
Alisema anaishauri
serikali kuanzisha sheria itakayozuia majengo ya kale kubomolewa na kuachwa
kama kumbukumbu.
“Kuna faida
kubwa za majengo kale kama wizara ya ,aliasili na utalii wakiwekea mkazo wa
kuyahifadhi na kuyatangaza,” alisema Aida.
Alisema moja
ya faida kubwa ni kuongeza vivutio vya watalii ambao wengi hupenda kutembelea
majengo ya kale.
“Majengo
kale yamekuwa yakitumika vema kule Zanzibar kwani yamekuwa yakiingiza theruthi
mbili ya pato la taifa,” alisema Aida.