HALMASHAURI
ya Jiji la Dar es Salaam imepanga kutumia shilingi milioni 463 katika
kukifanyia ukarabati kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo.
Akizungumza
na FICHUA, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita
alisema jiji limepitisha mpango wa manunuzi ambao utaruhusu kuanza kwa
ukarabati huo.
Alisema
ukarabati huo utahusisha ujenzi wa mifumo ya maegesho, vyoo, milango ya
kuingilia na taa.
“Jana
(Juzi)tumepitisha mpango wa manunuzi ambao tuna mamlaka ya kuanza kazi, na inawezekana
kesho(leo) mkaona zabuni zikitangazwa katika gazeti la serikali ambazo
zitajumuisha ujenzi wa maegesho, ” alisema Mwita.
Alisema
sambamba na hilo wanatarajia kuanza kwa ujenzi wa vituo vitatu vya mabasi
yaendayo mikoani na nje ya nchi katika maeneo tofauti.
“Ujenzi huo
utakaofanyika kwa ushirikiano wa serikali na sekta binafsi katika maeneo ya
Mbezi Luisi kwa mabasi ya mikoa ya kati na magharibi, Boko Basihaya kwa mikoa
ya kaskazini na Kongowe kwa mikoa ya kusini.
Mwita
alisema kupanda kwa viingilio vya wasindikizaji katika stand ya ubungo kutoka
shilingi 200 hadi 300 kunatokana na kupanda kwa gharama za maisha.
“Bei hizi
zilikuwapo tangu mwaka 1998 ni tofauti na sasa, na Faida za kuongezwa kwa
shilingi mia matunda yake yataonekana baadaye kwa kupata huduma zilizo bora,”
alisema Mwita.
Aidha
alisema wako katika mikakati ya kuweka kulipanga upya jiji la Dar es Salaam
ambapo tayari wameanza kufanya uchambuzi.
“Kwa sasa
wanaendelea kufanya tathmini kwa kutumia picha za ndege hivyo kufikia Septemba,
Mwaka huu tunaweza kutoa ‘masterplan’,” alisema Mwita.
mwisho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni