TAHARUKI imetanda katika maeneo ya Kivuko cha
Feri, jijini Dar es Salaam baada ya kudaiwa kivuko cha MV Magogoni kukwama najini na kupoteza uelekeo kutokana na upepo mkali uliokuwa ukivuma jana
asubuhi katika Bahari ya Hindi.
FICHUA ilifika maeneo hayo na kukuta baadhi ya wananchi wakielezea tukio
hilo ambao walidai kivuko hicho kilipoteza mwelekeo na kusababisha taharuki kwa
wananchi wanaotumia usafiri huo.
“
Kuna kivuko leo kilikuwa kimepakia abiria kikasombwa na upepo na kupelekwa
umbali mrefu hadi walipopata msaada wa kuvutwa baada ya masaa matatu kuanzia saa moja hadi saatatu asubuhi,” alisema
mmoja wa shuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Asia Rajab.
Alisema
kivuko hicho kilikwama kwa muda wa masaa matatu hivyo kuleta usumbufu mkubwa kwa wasafiri wanaotumia usafiri huo.
Alisema
hali hiyo imewafanya abiria kuogopa kukitumia kivuko hicho kwa hofu ya kuzama
majini.
Hata
hivyo Ofisa Habari wa TEMESA Theresia Mwami alikiri kupata taarifa hizo na
kudai kuwa wanazifanyia kazi na watatoa
taarifa itakapokuwa tayari.
Wakati
huohuo, Mamlaka ya Hali ya Hewa (Tma), jana imetoa tahadhari wananchi wa Ukanda
wa Pwani kwakuwa kutakuwa na upepo mkali unaozidi Km 40 kwa saa na mawimbi
makubwa katika bahari ya Hindi.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Tma, Dk.Agnes Kijazi
amesema vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika Mikoa ya Lindi, Mtwara,
Morogoro (Kusini) na Ruvuma.
Dk.Kijazi
alisema pia viwango vya joto , mawio na machweo ya jua kwa baadhi ya miji hapa
nchini vitabadilika.
“Kutakuwa na hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo na
vipindi vifupi vya jua,”alisema Dk Agnes.
Alisema
upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 40 kwa saa, kutoka
Kaskazini-Mashariki kwa Pwani ya
Kaskazini na kutoka Kaskazinikwa Pwani ya Kusini.
mwisho
karibuni kwa maoni
JibuFuta