Alhamisi, 17 Mei 2018

wakaguzi wa ndani waiangukia serikali


TAASISI ya Wakaguzi wa Ndani (IIA) Tanzania imeiomba serikali kufuata mwongozo wa kimataifa wa weledi wa ukaguzi wa ndani (International Professional Practice Framework) ili kuwawezesha kazi zao kutambulika kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa IIA Tanzania, Kafaso Millinga alisema kufuata mwongozo huo kutasaidia Wakaguzi wa Ndani kupata fursa za kufanya kazi hizo katika nchi mbalimbali.
"Tunaiomba serikali kuona umuhimu wa kuufuata mwongozo huu ambao utawasaidia wakaguzi wa ndani kutambulika kimataifa," alisema Millinga.
Alisema katika mwezi wa Mei ambao ni wa kujenga uelewa hivyo wameandaa mihadhara itakayofanyika katika vyuo na taasisi mbalimbali za elimu ili kujenga uelewa wa jamii kuhusu fani hiyo.
"IIA imeandaa mihadhara itakayofanyika katika Chuo kikuu cha Ardhi (ARU), Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM).
"Lengo ni kuuelimisha umma umuhimu wa wakaguzi wa ndani ili kuimarisha maendeleo ya kiuchumi kwa ngazi zote za taifa," alisema Millinga.

alisema pamoja na kutembelea vyuo hivyo pia watakutana na wadau mbalimbali wa maendeleo kuwajengea uelewa juu ya fani hiyo.
Alitoa rai kwa jamii kujifunza na kufuatilia taarifa na ripoti mbalimbali zinazotolewa na Wakaguzi wa ndani ili waweze kupata taarifa sahihi.
"Fani ya ukaguzi wa ndani inahitaji uwajibikaji na uadilifu wa hali ya juu hivyo tunahitaji umma wa watanzania kutupa ushirikiano katika kutekeleza majukumu," alisema Millinga.
Mwisho


Alhamisi, 22 Machi 2018

kipindupindu burahati kwa heri


-DAR ES SALAAM
WAKAZI wa Kata ya Mburahati, Manispaa ya Ubungo, jijini Dar es Salaam wataondokana na magonjwa ya mlipuko baada ya kuanza kwa ujenzi wa mradi wa uondoshaji maji taka katika kata hiyo.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi, Mhandisi mradi kutoka Borda ambao ndio wajenzi, Modekai Sanga alisema mradi huo ukikamilika utawanufaisha wakazi 40,000 wa Mburahati na maeneo jirani.
Alisema wakazi hao watapata huduma ya uondoshaji wa majitaka kwa gharama nafuu na hivyo kuondokana na magonjwa yatokanayo na uchafuzi wa mazingira hususani majitaka.
“Katika mradi huu kutapatikana nishati ya gesi ambacho ni lita 7,000 kwa siku, Mboji na maji ya kumwagilia bustani na miti,” alisema Sanga.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori alisema serikali inaendeleza juhudi za ujenzi wa miradi mbalimbali ya kuondosha majitaka kwa kushirikiana na wadau.
Alisema lengo la serikali ni kuwapatia wakazi wa jiji hilo huduma ya uondoshaji majitaka kwa asilimia 30 hadi kufikia mwaka 2020.
“Miradi hiyo ni uboreshaji na upanuzi wa mfumo wa maji taka kwa jiji la Dra es Salaam ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mitambo mitatu ya kisasa ya kusafishia maji katika maeneo ya Jangwani (mita za ujazo 200,000),” alisema Makori.
Aliongeza kuwa miradi mingine ni ule wa Kurasini ambao utakuwa na uwezo wa kuondosha majitaka  mita za ujazo 11,000 na wa Mbezi Beach (16,000).
Akizungumzia mradi wa uondoshaji maji Mburahati Makori alisema Ofisi ya Mkoa huo ilisaini makubaliano na shirika lisilo la Kiserikali la Borda la nchini Marekani kujenga mradi huo.
“Mapenda niwapongeze Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(Dawasa) kwa kushirikiana na Borda kutekeleza mradi huu ambao utawanufaisha wakazi wa Mburahati,” alisema Makori.
mwisho  

Jumapili, 25 Februari 2018

tumieni bidhaa za viwanda vya ndani

na tunu nassor



WATAALAMU wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji wameshauriwa kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini katika kutekeleza miradi ya maji ili nchi kuangalia mikataba wanayoingia ili nchi inufaike na miradi hiyo.
Akizungumza katika ziara aliyoifanya jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso alisema wataalamu hao waangalie mikataba wanayoingia ili kuruhusu baadhi ya vifaa vya ujenzi kununuliwa nchini.
Alisema kwa sababu nchi hii kwa sasa ni ya viwanda hivyo ni vyema wanapoingia mikataba kuondoa vipengele vitakavyowafunga katika kununua baadhi ya vifaa.
"Si busara vifaa kama koki na pampu kununuliwa nje ya nchi wakati vinapatikana hapa nchini,” alisema Aweso.
Alisema kwa kufanya hivyo kutasaidia kuongeza mitaji katika viwanda vya ndani, ajira na kuongeza mzunguko wa fedha nchini.
"Pamoja na kuwa na nia njema ya kuwapatia wananchi maji safi na salama lakini pia waliangalie hili kwa manufaa ya nchi,” alisema Aweso.
Aidha aliongeza kuwa bado kuna changamoto ya kuwapo kwa makandarasi wasiokidhi vigezo ambao hutekeleza miradi chini ya kiwango.
“Bado tuna changamoto ya makandarasi wanaopewa miradi 'kiushemeji shemeji' jambo ambalo linasababisha kushindwa kuteteleza kwa kiwango hivyo kama wizara tutawatapisha fedha hizo na kuzirudisha katika miradi," alisema Aweso.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(Dawasa), Modester Mushi alisema wanatarajia kuwaunganishia maji wateja 376,000 katika visima vya Mpera na Kimbiji.
Mwisho

dawasa, dawasco pelekeni maji pembezoni mwa mji


Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ameziagiza DAWASA na DAWASCO kuhakikisha zinafikisha huduma ya maji kwenye maeneo yaliyo pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam, ambapo kuna uhaba mkubwa wa maji pamoja na kuwa na wakazi wengi zaidi na si kujikita katikati ya jiji hilo tu.Naibu Waziri Aweso ametoa agizo hilo akiwa katika ziara ya kikazi katika Wilaya ya Temeke kujionea uhalisia wa utekelezaji wa miradi ya maji, wilaya ambayo imekuwa na malalamiko mengi kuhusiana na huduma hafifu ya majisafi  na salama.Aweso amesema kuwa kuna haja ya DAWASA na DAWASCO kuimarisha huduma ya maji kwenye maeneo ya pembezoni mwa jiji kama Temeke, Kigamboni, Ukonga, Mbagala na Segerea ili kukidhi mahitaji makubwa ya maji kwa wakazi wengi wanaoishi maeneo hayo.''Fanyeni utaratibu wa kukarabati miradi ya zamani kama hatua ya kwanza na ya haraka ya kuwapatia wananchi maji, wakati mkiendelea kutekeleza miradi mipya na mikubwa ambayo utekelezaji wake utachukua muda mrefu. Mmejikita sana katikati ya jiji, ambapo kwa sasa huduma hiyo imeimarika kwa kiasi kikubwa. Umefika wakati wa kuwekeza maeneo ya pembezoni kwa sasa, na wakazi hawa nao wafurahie huduma ya maji ya uhakika'', aliagiza Naibu Waziri Aweso.Aidha, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji alitoa onyo kwa manispaa zote za Jiji la Dar es Salaam kutowapa kazi wakandarasi wasio na uwezo. Pia, kuchukua hatua stahiki kwa wakandarasi wote wanaosuasua katika utekelezaji wa miradi, huku akiwahakikishia wakandarasi wote kulipwa fedha zao kwa wakati ili wasikwame katika